Mwananchi tayari umekata tiketi yako? Jumapili ya wiki hii kampeni ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika inaanza pale uwanja wa Azam Complex
Ni mchezo wa kwanza wa hatua ya awali dhidi ya Asas Fc ya Djibout. Hii ni mechi ambayo Yanga imedhamiria kuzitumia salamu timu zinazoshiriki ligi ya mabingwa msimu huu
Wale wanaodhani Yanga ilibahatisha kucheza fainali ya kombe la Shirikisho msimu uliopita, msimu huu wana 'surprise' nyingine katika michuano ya ligi ya mabingwa
Mkakati wa kwanza ni kutinga hatua ya makundi ambapo Wananchi wanahitaji kupata ushindi wa jumla katika mechi nne za kuelekea makundi
Mechi mbili ni dhidi ya Asas Fc na kufuatiwa na mechi nyingine mbili dhidi ya Otoho (Congo) au El Marreikh (Sudan).
Tuanza na hatua ya awali, tuwamalize Asas Fc pale Azam Complex Jumapili kabla ya mchezo wa marudiano ambao utapigwa Jumapili itakayofuata, August 28
