Hii Yanga kama una pumzi 'kisoda' utaumia

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
21 Aug 2023
Hii Yanga kama una pumzi 'kisoda' utaumia

Baada ya kuishuhudia Yanga katika mechi tatu za ushindani, kuna mabadiliko ya kiuchezaji kati ya sasa na ilivyokuwa msimu uliopita chini ya kocha Nasreddine Nabi

Kama ni kwenye ujenzi, Nabi alitengeneza msingi, sasa Miguel Gamondi anakamilisha ujenzi wa nyumba

Katika misimu ya karibuni kwenye soka la Tanzania, haijawahi kushuhudiwa timu inayocheza soka la kushambulia katika kiwango ambacho Yanga wanafanya

Nafikiri kigezo cha kwanza ambacho Gamondi anatumia pale anapopanga kikosi chake, lazima mchezaji uwe fit na tayari kukimbia sana uwanjani

Kwa aina hii ya uchezaji ipo siku kuna timu itashushiwa mzigo wa magoli! Yanga ya Gamondi ni marufuku kwa timu pinzani kumiliki mpira hata kwa sekunde 30

Timu inapopoteza mpira utaona wachezaji wanavyohaha kuurudisha kwenye himaya yao haraka

Kwa aina ya 'intensity' ambayo Yanga wanacheza nayo, ni timu chache sana ambazo zinaweza kuhimili kwa dakika zote 90

Jambo pekee ambalo Gamondi anahitaji kulifanyia kazi ni umaliziaji. Kama Yanga itatumia angalau nusu ya nafasi wanazotengeneza basi kila mechi watakuwa wakiondoka na ushindi mnono

Tumezoea timu nyingi huanza mchezo taratibu na kumaliza kwa kasi au kuwa na vipindi vya umiliki wa mchezo lakini ni tofauti kwa Yanga. Inavyoanza ndio hivyo hivyo itakavyomaliza

Jana katika mchezo dhidi ya Asas Fc, zilifika nyakati Asas licha ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0, walilazimika kujiangusha, kupoza mashambulizi na kupoteza muda maana sio kwa 'moto' waliokuwa wakipelekewa...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’