Mabingwa watetezi ligi kuu ya NBC Yanga leo wanaanza rasmi kampeni ya kubakisha ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo
Ni katika mchezo wao wa kwanza kwenye ligi kuu msimu huu wakiwa wenyeji wa KMC uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Utakuwa mchezo wa kwanza wa ligi kwa Kocha Miguel Gamondi na baadhi ya wachezaji waliosajiliwa katika dirisha hili la usajili linalotarajiwa kufungwa August 31
Baada ya kupoteza Ngao ya Jamii, Gamondi anafahamu ana kazi ya kulinda taji la ligi kuu pamoja na taji la Shirikisho la Azam (ASFC)
Hautakuwa mchezo mwepesi kwani hata KMC nao wameimarisha kikosi chao wakiwa na kocha Moalin aliyewahi kuinoa Azam Fc
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa leo ndio msimu wa burudani katika ligi kuu unaanza rasmi
Amewataka mashabiki wa Yanga kukata tiketi zao mapema na kuwahi Azam Complex kwani timu yao imewaandalia burudani ya aina yake
Mchezo utapigwa saa 1 usiku...