Yanga ya Gamondi unafungwa na kila mchezaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Aug 2023
Yanga ya Gamondi unafungwa na kila mchezaji

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ni kama ameanza kuwapa majibu wale waliokuwa na hofu kuwa timu yake inakabiliwa na mapungufu kwenye safu ya ushambuliaji

Jana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 ambayo yalifungwa na wachezaji watano tofauti

Dickson Job, Stephane Aziz Ki, Hafiz Konkoni, Mudathir Yahya na Pacome Zouzoua walifunga mabao hayo

Katika mchezo huo yalionekana mabadiliko makubwa ya kimbinu hasa pale Yanga iliposhambulia. Sio chini ya wachezaji watano waliingia katika eneo la hatari

Aidha matumizi ya Aziz Ki na Zouzoua yameanza kulipa kwani wawili hao walikuwa chachu ya ushindi huo mkubwa wa Yanga katika mchezo wa kwanza

Aziz Ki alianza kama winga wa kushoto huku Pacome akitumika kama namba 10, wawili hao walikuwa wakibadilishana majukumu uwanjani na kuwachanganya walinzi wa KMC

Uwezo wao mkubwa wa kupiga pasi elekezi ulifanya maisha kuwa rahisi kwa walinzi wa pembeni Nickson Kibabage na Yao kukimbia katika nafasi

Kuna kila dalili msimu huu vinara wengi wa kupachika mabao wataonekana kulinganisha na msimu uliopita ambao Fiston Mayele alifunga mabao mengi peke yake

Aidha Mudathir Yahya ameendelea kuwa mchezaji muhimu katika eneo la kiungo sambamba na Khalid Aucho

Chini ya Gamondi katika mechi chache tu, Mudathir amekuwa bora sana pengine zaidi ya kile alichofanya wakati wa Nabi

Gamondi amempa Mudathir uhuru wa kucheza kila mahali uwanjani, ni mchezaji mwenye 'energy' kubwa sana

Jambo pekee ambalo atahitaji kulifanyia kazi ni kwenye umaliziaji kwani ni mchezaji ambaye anakuwa katika maeneo sahihi ya kufunga lakini mashuti yake mengi hupaa langoni ukiacha goli alilofunga jana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’