Kiungo mshambuliaji wa Yanga Skudu Makudubela amerejea nchini akitokea Afrika Kusini kushughulikia hati ya kusafiria
Skudu amerejea Alfajiri ya leo Jumamosi akiwa na familia yake
Baada ya kutua, nyota huyo ameeleza kuwa na shauku kubwa ya kurudi uwanjani kuwatumikia Wananchi
"Nafuraha kubwa nimerejea, nilikuwa nafuatilia kila kinachoendelea hapa, juzi tulimpiga mtu tano, inahamasisha, sitasubiri kurejea uwanjani"
"Naendelea vizuri sasa, nimepata matibabu nafikiri Jumatatu daktari wa timu atatoa ripoti ila nina hamu kubwa ya kurejea uwanjani kuonana na mashabiki wetu bora 'Wananchi'," alisema Skudu
ADVERTISE HERE