Gamondi ametega mabomu, yatawalipukia wengi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Aug 2023
Gamondi ametega mabomu, yatawalipukia wengi

Katika mechi sita ambazo Yanga wamecheza msimu huu chini ya Kocha Miguel Gamondi kuna utofauti mkubwa wa uchezaji umeonekana

Yanga ilianza taratibu lakini kasi imeendelea kuongezeka kutoka mchezo mmoja hadi mwingine

Yanga ya Gamondi sio tu inakupigia mpira mwingi, lakini pia haikupi nafasi ya kucheza na ukikaa vibaya utaokota sana mipira katika nyavu zako

Katika mechi mbili zilizopita, mabao 10 yamefungwa, KMC alipigwa mkono na jana Asas Fc akapigwa mkono mwingine

Katika mechi sita Yanga imeruhusu bao moja tu ndani ya dakika 90. Bao hilo lilifungwa jana kwenye mchezo dhidi ya Asas Fc kwa mkwaju wa penati baada ya Zawadi Mauya kufanya madhambi ndani ya eneo la hatari

Gamondi alichukizwa na timu yake kuruhusu bao hilo, akibainisha kuwa wanafanya kazi kubwa katika kiwanja cha mazoezi kuhakikisha wapinzani wao hawafungi

Wachezaji wote wa Yanga wameiva, anayecheza ni moto na aliyebenchi pia ni moto

Iko siku Gamondi anaweza kumpa kazi kocha wa timu pinzani achague mwenyewe kikosi cha kucheza nacho na bado akakutana na adhabu kali ndani ya dakika 90

Yanga ya Nasreddine Nabi ilikuwa bora lakini hii ya Gamondi kuna kitu zaidi kimeongezeka kwani wachezaji wako tayari kukimbia kwa dakika zote 90

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’