Matchday : Yanga vs JKT Tanzania, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Aug 2023
Matchday : Yanga vs JKT Tanzania, NBC PL

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa ambapo mabingwa watetezi Yanga watashuka uwanja wa Azam Complex, kumenyana na JKT Tanzania

Utakuwa mchezo wa pili kwa Yanga msimu huu, Wananchi wakianza ligi kibabe kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa kwanza

Matarajio ya Wananchi ni kuona timu yao ikiibuka na ushindi leo ambapo ushindi wa kuanzia mabao mawili 2-0 utaipeleka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi

Baada ya Azam Fc kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Prisons jana, walikaa kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama sita, mabao 7 ya kufunga na kuruhusu bao 1

Hata hivyo ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi kwani  JKT Tanzania inayonolewa na kocha Malale Hamsini, imesheheni wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa ligi

Timu hiyo iliyopanda daraja msimu uliopita, asilimia 90 ya wachezaji wapya waliowasajili wameshiriki ligi kuu kwa muda mrefu

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema hawatawadharau wapinzani wao lakini wataingia katika mchezo huo kwa lengo moja tu, kuzisaka alama zote tatu ili kuwapa furaha mashabiki wao ambao  wamekuwa na sapoti kubwa kwa timu yao

Mchezo utapigwa kuanzia saa 1 usiku..

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’