Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki kwa mara nyingine leo anatarajiwa kuwaongoza Wananchi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania
Mchezo huo utapigwa saa 1 usiku katika uwanja wa Azam Complex
Aziz Ki ni kama amezaliwa upya msimu huu akihusika kwenye kila ushindi ambao Yanga wamepata
Anafunga, anatoa pasi za mabao lakini pia anatoa burudani kwa mashabiki
Huenda JKT Tanzania wakakumbana na kile walichokumbana nacho KMC hasa kama Kocha Miguel Gamondi atawatumia pamoja Aziz Ki, Maxi Nzengeli na Pacome Zouzoua 'Zizou'
Aziz Ki yuko fit, imara na tayari kutumika dakika zote 90 za mchezo
Mwenyewe anasema msimu wake wa kwanza hakufanya kile ambacho Wananchi walihitaji kutoka kwake, sasa msimu huu amepania kuwapa furaha
ADVERTISE HERE