Yanga hii, wapinzani watateseka sana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Aug 2023
Yanga hii, wapinzani watateseka sana

Wananchi wana raha msimu huu, wacha watambe! Kwa sababu wana timu bora yenye wachezaji wa daraja la juu

Kuna mashabiki wa timu moja walikuwa wakitamba sana wakati wa usajili, lakini sasa hivi wako kimyaaaa

Licha ya kushinda mechi zao bado wanashinikiza Kocha wao afukuzwe!

Haya yote yanatokea baada ya kuwashuhudia Wananchi wakicheza soka la kutisha na kugawa vipigo katika mechi zao

Hivi mara ya mwisho umesikia lini timu imeshinda mechi tatu mfululizo kwa ushindi wa mabao matano?

Imefika wakati mashabiki wa Yanga wanalalamika kuwa muda wa dakika 90 hautoshi!

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi na benchi lake la ufundi wamefanya kazi kubwa katika kiwanja cha mazoezi na sasa matunda yake yanaonekana

Yanga hii inacheza dakika 90 kwa kasi ileile, utimamu wa wachezaji ni wa kiwango cha juu sana

Huu unaweza kuwa msimu wa kihistoria kwa Yanga kama wataendeleza kasi hii. Kuna uwezekano Wananchi wakamaliza msimu na zaidi ya mabao 100 kama mechi mbili tu tayari wana mabao 10

Zile tuzo za kila mwezi Kocha bora na mchezaji bora huenda zote zikaishia Jangwani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’