Mlinzi wa kati wa Yanga Gift Fred na kiungo Khalid Aucho walijumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda kitakachocheza na Niger Septemba 07 katika mchezo wa kuwania tiketi ya fainali ya michuano ya Afcon 2023
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema walitaarifiwa na Shirikisho la Soka Uganda kuwa Fred alipata majeraha kwenye mazoezi ya timu hiyo, wamemruhusu arejee klabuni
"Gift Fred ni miongoni mwa wachezaji wetu (12) walioitwa kwenye timu mbalimbali za taifa. Fred akiwa kwenye mazoezi na timu yake ya taifa ya Uganda alipata minor injury (Injury ndogo) ambayo ingemuweka nje kwa siku 3 hadi 4"
"Madaktari wa timu ya taifa ya Uganda wametutaarifu kuwa wamemruhusu Gift Fred kurejea Tanzania na kocha ameshaita mbadala wake kuelekea mechi yao ya kufuzu AFCON dhidi ya Niger"
"Kikosi kimetoka jana public tayari Fred alikuwa ameshaondolewa kwenye squad baada ya kupata injury. Hivyo Fred anarejea nchini.Taarifa kwamba hakuitwa ni uongo kwani call-ups zote za wachezaji kwenye timu zao za taifa hupitia (TFF)," alisema Kamwe