Yanga Princess kushiriki mashindano maalum Dodoma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Sep 2023
Yanga Princess kushiriki mashindano maalum Dodoma

Kikosi cha Yanga Princess kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Wanawake na mashindano ya Get International, huku akisisitiza kuwa wanataka ubingwa

Wiki iliyopita Yanga Princess iliachana na wachezaji 13, imefanya usajili bora zaidi unaowajumuisha nyota  wa kigeni akiwemo Madina Traore kiungo kutoka Burkina Faso, Faiza Sedu straika raia wa Ghana na Adejoke Ejalonibu kiungo mshambuliaji kutoka Raja Casablanca ya Morocco.

Kocha Msaidizi wa Yanga Princess Fred Mbuna amesema viongozi wa Yanga waliona haja ya kuondoa wachezaji 13 ili kuimarisha kikosi kwa ajili ya msimu ujao na anaamini wapya waliosajiliwa watasaidia kutwaa ubingwa

Msimu uliopita Yanga Princess ilimaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Yanga Princess ilicheza mechi mbili za kirafiki wiki iliyopita ile ya kwanza ikishinda mabao 7-0 dhidi ya Sports Academy na 2-0 dhidi ya Ilala Queens ikiwa ni kipimo cha maandalizi ya michuano ya Get International yatakayofanyika mjini Dodoma kuanzia Septemba 9 hadi 23.

Mashindano hayo yanajumuisha timu 12 zikiwamo Get Program, Fountain Gate Princess, Yanga Princess, Simba Queens, Bunda Queens, New Generation, JKT Queens, Alliance Girls, CFC Aman FC, Polisi Queens, Kampala Queens na Ceasia Queens.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’