Waliokuwa Stars kuripoti kambini Jumatatu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Sep 2023
Waliokuwa Stars kuripoti kambini Jumatatu

Baada timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kurejea nchini kutoka Algeria ambako walifanikiwa kufuzu michuano ya Afcon 2023, nyota wa Yanga waliokuwa kwenye kikosi hicho wanatarajiwa kurejea kambini Jumatatu kuendelea na maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa

Jumamosi ijayo, Septemba 16 Yanga itakuwa Rwanda kuchuana na AL Merrikh katika mchezo wa mkondo wa kwanza

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Miguel Gamondi alitoa mapumziko kwa siku ya leo Jumapili

Aidha Kamwe amesema Yanga inafanya utaratibu wa kumsafiri kiungo Stephane Aziz Ki ambaye yuko Morocco na timu ya Taifa ya Burkina Faso

"Kocha (Gamondi) alitoa mapumziko kwa wachezaji wote siku ya leo hivyo tunatarajiwa hapo kesho wote ikiwa ni pamoja na wale waliokuwa katika majukumu ya timu ya Taifa wataripoti mazoezini"

"Kuhusu kiungo wetu Stephane Aziz Ki ambaye yuko Morocco ambako walipaswa kucheza dhidi ya Morocco lakini mchezo huo umeahirishwa kutokana na tetemeko la arhi lililokumba nchi hiyo"

"Tumewasiliana nae, yuko salama na wachezaji wenzake wa Burkina Faso, uongozi umewasiliana na FA ya Burkina Faso na tunaandaa utaratibu kuhakikisha Aziz Ki anarejea nchini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Al Merrikh," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’