Wakati Yanga ikijiandaa kuikabili Welayta Dicha kwenye mchezo wa kwanza wa kusaka tiketi ya kutinga makundi kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaopigwa uwanja wa Taifa Jumamosi April 07 2018, itawakosa Obrey Chirwa, Said Juma Makapu na Papi Tshishimbi kwenye mchezo huo.
Wachezaji hao wote wamefikisha kadi mbili za njano baada ya kupata kadi kwenye mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo yanayosimamiwa na CAF, wanapaswa kukosa mchezo mmoja.
Adhabu kama hiyo ilimkumba beki Hassani Kessy ambaye alikosa mchezo dhidi ya Township Rollers.
Hata hivyo kurejea kwa Donald Ngoma kikosini kumeipa ahueni Yanga kuelekea mchezo huo wa kwanza utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Aidha kukosekana kwa Tshishimbi na Makapu kwenye mchezo huo huenda kukawapa nafasi chipukizi Maka Edward, Thabani Kamusoko na Pato Ngonyani kuweza kurejea kwenye kikosi cha kwanza.

ADVERTISE HERE