Kiungo fundi wa Yanga Salum Abubakar 'Sure Boy' anatarajiwa kusaini mkataba mpya kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa nchi
Mkataba wake wa awali wa miaka miwili unatarajiwa kufikia tamati mwezi Disemba mwaka huu uongozi wa Yanga ukiwa tayari umeanza nae mazungumzo ya mkataba mpya
Misimu yake miwili na Yanga imekuwa ya mafanikio makubwa akiwa sehemu ya kikosi kilichoshinda mataji sita pamoja na kucheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika msimu uliopita
Wengi wanakumbuka kiwango bora alichoonyesha katika mchezo dhidi ya Club Africain uliopigwa Tunisia na kuipeleka Yanga hatua ya makundi ya Shirikisho
Sureboy pia alin'gara katika mechi zote ambazo Yanga ilicheza na 'Waarabu' katika mashindano hayo
ADVERTISE HERE