Yale mashindano ya Gates International Tournament yameanza mkoani Dodoma ambapo Yanga Princess leo itashuka uwanja wa Shell Complex Chinangali kuikabili New Generation Fc
Ni mashindano yanayokutanisha timu zinazoshiriki ligi kuu ya Wanawake na baadhi ya timu za Wanawake kutoka nchi jirani
Mashindano hayo yameandaliwa na Fountage Gate Princess yakitumika kama sehemu ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya Wanawake, 2023/24
Meneja wa Yanga Princess Abbas Sykes amesema wako mkoani Dodoma wakiwa na dhamira moja tu, kutwaa taji la mashindano hayo
Yanga Princess kwa sasa inanolewa na kocha mpya raia wa Zambia, Haalubono Charles
ADVERTISE HERE