Akijibu maswali ya waandishi wa Habari jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga Hussein Nyika amesema mshambuliaji raia wa Zimbabwe Donald Ngoma atarejea rasmi kwenye kikosi cha Yanga kesho Alhamisi Yanga itakapoanza maandalizi ya mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Singida United.
Nyika alisema Daktari wa Yanga amewathibitishia kuwa Ngoma amepona kwa asilimia 100 na sasa yuko tayari kurejea kikosini.
Ngoma amekuwa akifanya mazoezi ya peke yake kwa takribani wiki mbili ikiwa ni hatua ya awali ya kumuwezesha kurejea dimbani kwa usalama.
Kurejea kwa Ngoma kunaimarisha zaidi safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo imekuwa ikiwategemea Obrey Chirwa na Pius Buswita.

ADVERTISE HERE