Gamondi agawa tuzo kwa wachezaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Sep 2023
Gamondi agawa tuzo kwa wachezaji

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema tuzo aliyoshinda kuwa Kocha bora wa Ligi Kuu kwa mwezi August 2023 ni matunda ya kazi nzuri inayofanywa na wachezaji wake uwanjani

Gamondi alishinda tuzo hiyo ya kwanza msimu huu baada ya kuingoza Yanga kushinda mechi mbili za ligi kuu huku Wananchi wakifunga mabao 10

Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi August pia ilichukuliwa na mchezaji wa Yanga, Maxi Mpia Nzengeli

Gamondi amewapongeza wachezaji kwa kufanya kile wanachoelekezwa kwa usahihi, tuzo hiyo ni matokeo ya kazi yao nzuri uwanjani

"Kwanza nawashukuru watu wote waliohusika katika kuhakikisha Yanga inapata matokeo mazuri mwezi Agosti, 2023 na hatimaye mimi kuchaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi"

"Nawapongeza wachezaji kwa kutekeleza vyema majukumu yao, sisi kama makocha sio chochote bila wachezaji," alisema Gamondi

Gamondi ameanza vyema majukumu yake katika kikosi cha Yanga mapema tu akijihakikishia ufalme wake mbele ya mashabiki kutokana na kandanda safi inayotandzwa na timu yake

Baada ya Nasreddine Nabi kuondoka, wapo waliokuwa na mashaka kama Yanga ingeweza kubaki na uimara wake kama ilivyofanya misimu miwili ya Nabi

Hata hivyo ni kama Yanga ya Gamondi imekuwa bora zaidi kuliko ile ya Nabi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’