Droo ya mtoano kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika imefanyika leo Cairo nchini Misri ambapo Yanga imepangwa kucheza na Welayta Dicha kutoka nchini Ethiopia.
Welayta Dicha ilipenya kwenye raundi ya kwanza kombe la Shirikisho kwa kuiondosha Zamaleki kwa mikwaju ya penati.
Welayta Dicha ilishinda 2-1 katika mchezo wa kwanza kisha ikachapwa 2-1 kwenye mchezo wa marudiano hivyo kupelekea changamoto ya mikwaju ya penati.
Ni hii hii Welayta iliyoponea chupuchupu kwa Zimamoto kwenye hatua ya awali ya michuano ya kombe la Shirikisho kwa kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 2-1.
Ilipata sare ya bao 1-1 Zanzibar kisha kushinda kwa bao 1-0 nyumbani kwao Ethiopia
Yanga imetinga hatua hiyo baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kwa kuchapwa mabao 2-1 na Township Rollers.
Welayta Dicha inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Ethiopia ikiwa imejikusanyia alama 19 kutoka michezo 15
Mchezo wa kwanza unatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Taifa kati ya April 06-08 na marudiano kupigwa nchini Ethiopia siku 10 baadae.

ADVERTISE HERE