Klabu ya Yanga leo imekabidhi mifuko 200 ya saruji na bati 70 kwa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), Kigali Rwanda
Ni katika kuwasaidia waathirika wa mafuruko yaliyotokea mwezi Mei mwaka huu maeneo ya Rubavu na Wilaya ya Rutsiro jimbo la Kaskazini na wilaya ya Burera jimbo la Kusini mwa Rwanda
Misaada hiyo imekabidhiwa na Rais wa Yanga, Hersi Said na kupokewa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa WFP tawi la Rwanda hapa jijini Kigali, Munyazikwiye Jerome
Yanga iko Rwanda ambapo kesho Jumamos itamenyana na Al Merrikh kwenye mchezo kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika
ADVERTISE HERE