Mlinda lango namba moja wa Yanga Djigui Diarra ni miongoni mwa wachezaji walioshiriki mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo dhidi ya Al Merrikh ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Pele, Kigali
Diarra alikuwa mchezaji wa mwisho kutua Rwanda akichelewa kutokana na kukabiliwa na majukumu ya timu ya Taifa
Juzi alishiriki mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Ivory Coast, akikaa langoni mwa dakika zote 90
Kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki alikuwa mchezaji wa kwanza kuwasili Rwanda ambapo jana aliwapokea wenzake waliotua kutoka Tanzania
Mchezaji pekee ambaye atakosekana hapo kesho ni nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye alibaki Tanzania kutokana na matatizo ya kifamilia
ADVERTISE HERE