Ni kivumbi na jasho Rwanda leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Sep 2023
Ni kivumbi na jasho Rwanda leo

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo wako nchini Rwanda wakikabiliwa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi, utapigwa kwenye uwanja wa Pele, Kigali saa 9 Alasiri (saa 10 Tanzania)

Ikisafiri na idadi kubwa ya mashabiki kutoka Tanzania, Yanga leo inaanza kampeni ya kuiondosha Al Merrikh katika michuano hiyo na kutinga hatua ya makundi

Ni takribani miaka 24 Yanga haijacheza hatua ya makundi, kikosi cha Kocha Miguel Gamondi kinasaka rekodi ya kuwarejesha Wananchi katika hatua hiyo baada ya muda mrefu

Msimu uliopita Yanga ilipata mafanikio makubwa katika michuano ya kombe la Shirikisho (CAF CC) ikicheza hatua ya fainali na kuvaa medali ya ushindi wa pili

Msiimu huu Yanga imejiwekea malengo ya kutinga hatua ya makundi, uongozi wa timu hiyo ukiamini kama watafanikisha malengo hayo, watakuwa na nafasi ya kufanya vizuri zaidi katika hatua itakayofuata

Yanga itashuka uwanjani leo kuikabili Al Merrikh ikiwa na kikosi chake kamili

Ni mchezaji mmoja tu, nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye hakusafiri Rwanda kutokana na matatizo ya kifamilia

Baada ya kuanza vyema mechi za hatua ya awali, matarajio ya Wananchi ni kuona timu yao ikiendeleza ubabe katika mchezo huo dhidi ya Al Merrikh

Kila la kheri Wananchi huko Rwanda....

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’