Klabu ya Yanga imeshinda mechi sita mfululizo ugenini katika mechi za CAF CL na CAF CC
Ushindi wa mabao 2-0 ambao Yanga wamepata dhidi ya Al Merrikh leo umewafanya Wananchi wawe na rekodi ya kutisha katika mechi za ugenini
Tangu ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TP Mazembe msimu uliopita katika michuano ya kombe la Shirikisho mchezo uliopigwa Lubumbashi, Yanga imeshinda mechi zote zilizofuata ugenini
Iliichapa Rivers United (2-0), Marumo Gallants (2-1(, USM Alger (1-0), Asas Fc (2-0) na leo Al Merrikh (2-0). Katika mechi zote Yanga iliruhusu bao moja tu ugenini
Sio kwa bahati mbaya Yanga kushika nafasi ya tatu katika ubora wa soka ngazi ya klabu barani Afrika
ADVERTISE HERE