Bado hatujafuzu Ligi ya Mabingwa - Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Sep 2023
Bado hatujafuzu Ligi ya Mabingwa - Gamondi

Pamoja na kikosi chake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Al Merrikh, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema bado hawajakata titeki ya kutinga hatua ya makundi na watahitaji kujiandaa vyema ili kuhakikisha wanashinda mechi ya marudiano itakayopigwa Septemba 30 katika uwanja wa Azam Complex

Aidha Gamondi amesema kwa sasa wanaweka nguvu katika mchezo wa ligi kuu unaofuata dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumatano, baadae watarejea Avic Town kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Merrikh ambao ndio utaamua hatma yao kuelekea hatua ya makundi

Hata hivyo Gamondi amewapongeza wachezaji wake kwa kuonyesha kiwango bora katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Pele Kigali, Rwanda na Yanga kushinda mabao 2-0

"Tulikuwa na dakika 90 nzuri, nawapongeza sana wachezaji wangu, licha ya ugumu wa mchezo hasa kipindi cha kwanza, ila walirudi kipindi cha pili na akili kubwa ya kutafuta ushindi na tukafanikiwa"

"Tunawaheshimu wapinzani wetu lakini nadhani tulistahili ushindi mkubwa zaidi ya huu kulingana na jinsi tulivyotengeneza nafasi za wazi"

"Mechi ya kwanza imekwisha, sasa tunatakiwa kuhamisha akili kwenye mechi ya ligi na baada ya hapo tutamalizana na wapinzani wetu hao wa CAF, nataka nikwambie bado hatujafuzu, ushindi mzuri unatakiwa kuwa mechi hii ya pili, hata wao wanaweza kutufunga kwetu kama hatutakuwa makini," alisema Gamondi ambaye alirejea nchini jana na kikosi cha Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’