Mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo Fc siku ya Jumatano ni Maalum kwa ajili ya Wananchi waliojitoa kusafiri na timu Rwanda kuongeza hamasa kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh, na kuweka rekodi ya kujaza uwanja wa Pele Kigali
Shabiki ni mchezaji wa 12 uwanjani hivyo heshima itatolewa kwenye dakika ya 12 kwa mashabiki wote waliosafiri Rwanda
Hili ni tukio la aina yake ambalo litajiri pale uwanja wa Azam Complex siku ya Jumatano katika mchezo dhidi ya Namungo Fc
Viingilio vya mchezo vimetangazwa na tiketi tayari zinauzwa kupitia mitandao ya simu na vituoni


ADVERTISE HERE