Kikosi cha Yanga kinaelekea Chamazi ambapo majira ya saa 1 usiku watashuka uwanja wa Azam Complex kuikabili Namungo Fc katika mchezo wa raundi ya 3 ligi kuu ya NBC
Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga kuzisaka alama zote tatu ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi
Aidha ni mchezo maalum kuwapa heshima mashabiki wote waliosafiri nchini Rwanda kuiongezea hamasa Yanga katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh ambao Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
Wakati mchezo ukiendelea, kutakuwa na tukio maalum la kusimama na kupiga makofi kwenye dakika ya 12 kwa Wananchi wote watakaokuwa uwanjani na hata wale ambao watabaki nyumbani na kwenye 'vibanda umiza'
Pasipo na shaka Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi leo atatumia silaha zake zote muhimu ili kuhakikisha alama tatu zinapatikana
Gamondi hajawahi kudharau mechi na amesisitiza kuwa jambo muhimu kwake ni ushindi pasipo kujali idadi ya mabao waliyofunga
Morali ya wachezaji wa Yanga iko juu wakwia tayari kuendeleza ubabe katika ligi kuu ya NBC