Kocha Al Merrikh akiri Yanga inatisha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Sep 2023
Kocha Al Merrikh akiri Yanga inatisha

Kocha Mkuu wa Al Merrikh Lee Clark amesema haikuwa rahisi kwao kukabiliana na Yanga katika mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Mchezo huo uliopigwa nchini Rwanda ulishuhudia Wananchi wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutinga makundi wakihitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare katika mchezo wa mkondo wa pili ambao utapigwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Azam Complex

Clark amesema kwa sasa Yanga ni moja ya klabu kubwa na zinazoogopwa barani Afrika kutokana na kile walichofanya katika michuano ya kombe la Shirikisho msimu uliopita

Hata hivyo amesema vijana wake watakuja Dar wakiwa na dhamira ya kushinda, licha ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0

"Yanga ni miongoni mwa timu zinazoogopwa kwa sasa Barani Africa, Sisi tutawaheshimu lakini hatutakaa nyuma, kama Yanga waliweza kupata magoli mawili ugenini hata sisi tunaweza kupata magoli mawili ugenini," alisema

Al Merrikh imekuwa na historia nzuri katika misimu sita iliyopita ikifanikiwa kucheza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Ni wazi bado mechi haijamalizika ambapo hata kocha wa Yanga Miguel Gamondi amesema wanafahamu mchezo wa marudiano utakuwa mgumu zaidi na hawafikirii matokeo waliyopata katika mchezo wa kwanza

"Bado hatujafuzu, tuna mechi nyingine ngumu nyumbani, tunajiandaa kikamilifu tunajua Al Merrikh watakuja kwa nguvu, hawana cha kupoteza hivyo tunapaswa kuwa makini kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi nyumbani," alisema Gamondi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’