Yanga imeanza msimu wa mashindano 2023/24 kibabe ikishinda mechi zote tatu za ligi kuu ya NBC na kufikisha alama 9
Alama tisa zilizoambatana na mabao 11 ya kufunga huku lango likibaki salama kwa asilimia 100
Walinda lango Metacha Mnata na Djigui Diarra walikaa langoni katika mechi hizo ambapo Metacha alidaka mechi dhidi ya KMC na Diarra akawa langoni katika mechi dhidi ya JKT Tanzania na Namungo Fc
Huu unaweza kuwa msimu mwingine kwa Diarra kubeba tuzo ya kipa bora wa ligi kuu ambayo anaishikilia kwa misimu miwili
Dakika 180 katika mechi mbili za ligi zimekuwa bora sana, akihakikisha analinda vyema lango la Yanga
Mlinda lango ndiye kiongozi katika safu ya ulinzi, Diarra amefanikiwa kuwa kiongozi bora na kuifanya safu ya ulinzi ya Yanga kuepuka makosa na kuepelekea kupata cleensheet tatu katika mechi nne za mashindano ambazo Diarra alikuwa langoni
Lakini pia ni msimu ambao Metacha na hata Aboutwalib Mshery watakuwa na nafasi ya kuonekana katika baadhi ya mechi
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameonyesha ana imani na wachezaji wake wote na sio muoga wa kufanya 'rotation'