Aziz Ki ataja siri ya mafanikio yake msimu huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Sep 2023
Aziz Ki ataja siri ya mafanikio yake msimu huu

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Aziz Stephanie Ki amesema kuwa kilichomfanya asifikie matarajio ya mashabiki wake msimu uliopita ilikuwa ni ugumu wa kuzoea mazingira mapya ya Tanzania baada ya kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast

Msimu uliopita Aziz Ki alihusika katika mabao 13 ya Yanga kwenye Ligi Kuu ya NBC akifunga mabao 9 na kutoa assits 4

Msimu huu mpaka sasa amehusika kwenye mabao 3, amefunga mabao mawili na assist moja katika michezo mitatu ya Ligi

"Siri ya mimi kuendelea kufanya vizuri msimu huu ni Mungu, sababu haya ni maisha na huwezi kuwa juu siku zote, kuna wakati unakuwa na siku mbaya hivyo unatakiwa kumshukuru Mungu na kusema asante kwa kila jambo"

"Unajua wakati unapohama Ligi moja kwenda nyingine kwa mara ya kwanza inakuwa ngumu kwa sababu unatakiwa ujifunze baadhi ya vitu, uzoee mazingira na hali ya maeneo husika"

"Msimu uliopita ulikuwa mzuri kwa sababu kulikuwa na nyakati nzuri na mbaya, huzuni na furaha, kwa hiyo nilijifunza soka la Tanzania na sasa nimezoea. Nina marafiki na pia tuna timu nzuri kila mmoja anajitoa, hivyo ni wakati wangu wa kufurahia soka," amesema Aziz Ki

Aziz Ki amebeba hamasa ya mchezo wa mkondo wa pili kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa kati ya Yanga dhidi ya Al Merrikh utakaopigwa Jumamosi, Septemba 30

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
1h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
13h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
22h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’