Pichani juu kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki akikabidhiwa funguo na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Damas Ndumbaro ambaye leo aliwatembelea wahezaji wa Yanga Avic Town wakikamilisha maandalizi ya mchezo dhidi ya Al Merrikh ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Azam Complex
Ki amemkaribisha Dk Ndumbaro kwenye 'Key Day', siku ambayo Wananchi wamedhamiria kutinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa kwa ushindi dhidi ya Al Merrikh
Waziri Ndumbaro aliambatana na Rais wa TFF Wallace Karia pamoja na viongozi waandamizi kutoka Wizarani na TFF, walitembelea Avic Town kushuhudia mazoezi ya mwisho ya Yanga pamoja na kuwapa hamasa wachezaji ili kuhakikisha wanashinda mchezo hapo kesho
Yanga imekamilisha mazoezi yake ya mwisho kuelekea mchezo huo wa kuamua hatma ya kufuzu makundi