Baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga inarejesha makali yake katika mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC
Leo Wananchi wanatarajiwa kusafiri mkoani Mbeya ambako siku ya Jumatano wanakabiliwa na mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Ihefu Fc
Mchezo huo utapigwa uwanja wa Highland Estate huko Mbarali nje kidogo ya jiji la Mbeya
Hii ni mechi ya kisasi kwa Yanga kwani Wananchi wanakumbuka msimu uliopita waliziacha alama zote tatu Mbarali na pia rekodi yao ya 'unbeaten' ikaishia kwenye mechi ya 49
Ihefu Fc wametangaza viingilio vya mchezo huo ambapo Mzunguuko ni Tsh 10,000/- na VIP ni Tsh 30,000/-
Yanga inakwenda Mbeya ikiwa na mkakati wa kuendeleza ubabe wake kwenye ligi baada ya ushindi katika mechi zote tatu zilizopita na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi