Ukipita kwenye mazoezi ya Yanga Princess yanayofanyika uwanja wa Uhuru, utamshuhudia nyota raia wa Marekani, Kaider Wilson
Kaider anajifua na Yanga Princess lakini anatarajiwa kuanza kutumika mwezi Disemba usajili wake ukitarajiwa kukamilishwa kwenye dirisha dogo
Wengi wamevutiwa na kiungo huyo mshambuliaji na hakuna shaka ataiongezea Yanga Princess makali
Kaider ameeleza furaha yake kusajiliwa na Yanga Princess akifichua kuwa hii ni mara yake ya kwanza kucheza soka barani Afrika
Kaider amesema anaamini atakuwa na msaada mkubwa katika kuhakikisha Yanga Princess inatimiza malengo yake msimu huu
"Ni mara yangu ya kwanza kucheza soka Afrika, sikuwahi kufikiria ila namshkuru sana Baba yangu kwa kunipambania. Najua ni muda mrefu sana timu yetu haijabeba ubingwa wa ligi ya wanawake lakini msimu huu ni wakwetu nawaahidi mashabiki tutafanya vizuri," alisema