Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Ihefu Fc jana, kikosi cha Yanga kinaelekea mkoani Mwanza ambako wanakabiliwa na mchezo mwingine wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold siku ya Jumamosi
Huu ni mchezo muhimu sana kwa Yanga kushinda ili kuepuka presha ya nje ya uwanja
Kimahesabu tayari Yanga iko nyuma ya watani zao Simba kwa alama tatu baada ya ushindi wao wa mabao 3-1 dhidi ya Prisons
Ni wazi kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamondi aliondoka na somo muhimu kule Mbarali na pasipo na shaka siku ya Jumamosi ataanza na kikosi chake cha ushindi
Yanga ilirejea jijini Dar es salaam jana usiku na ilitarajiwa kuelekea jijini Mwanza usiku leo
Unaweza kusema mchezo dhidi ya Geita Gold ni kama fainali kwani Wananchi hawatakuwa tayari kupoteza alama nyingine katika mchezo wa pili mfululizo