Tusichoke kulalamika kuhusu waamuzi - Manara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Oct 2023
Tusichoke kulalamika kuhusu waamuzi - Manara

Aliyewahi kuwa Afisa Mhamasishaji wa Yanga Haji Manara amesema wadau wa soka ni wajibu wao kuendelea kulalamika kile kinachoendelea kwenye ligi kuu kwa maamuzi ya kustaajabisha kwenye baadhi ya mechi

Manara ametoa kauli hiyo baada ya mchezo kati ya Singida BS dhidi ya Simba uliopigwa jana kwenye uwanja wa LITI na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 huku kukiwa na malalamiko kuwa Singida BS walikataliwa bao halali walilofunga huku ikidaiwa kuwa bao la pili walilofunga Simba mfungaji aliotea

Manara amesema umefika wakati kwa wenye mamlaka ya soka nchini kushughulikia changamoto ya waamuzi kwani haileti taswira nzuri katika soka la Tanzania

Manara amesema kibaya zaidi matukio hayo yamekuwa yakiinufaisha zaidi timu moja kwani katika mechi tano walizocheza, matokeo ya mechi tatu yaligubikwa na maamuzi yenye utata

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Manara ameandika ujumbe huu;

Marehemu Gratian Matovu,Hafidh Ally Tahir,Juma Ally David,Msafiri Mkeremi,Na nisimsahau Meja Gwaza Mapunda aliyepata kuwa Referees Instructor wa FIFA.

Hao ni sehemu ya Waamuzi wachache wa zamani wa Kimataifa ambao waliipa heshma kubwa hii Nchi kwa kuchezesha mashindano makubwa ya kimataifa, zikiwemo Afcon na Tournaments nyingine kubwa kubwa!!

Sijui kama mnajua Marehemu Hafidh Ally alipata kuchezesha hadi fainali za Dunia za Under 17 na 20?

Leo mshajiuliza tunakwama Wapi Waamuzi wetu kupewa mashindano makubwa kuchezesha ? Mnadhani FIFA na CAF hawayaoni haya madudu yao ya huku? Ukubwa wa nchi yetu inakuwaje Waamuzi wetu hawapati hizi fursa?

Tusipokuwa Serious na hili jambo kuna siku tutavuna mabua itakuwa mbaya sana, kila siku complains hizi hizi tu, hatuoni aibu ndugu zangu?

Ni kweli yapo makosa ya kibinaadamu lakini kwa Waamuzi wetu kurejea rejea makosa sio makosa ya kibinaadamu ni kusudi 100%

Na niwaambie hizi sifa za Ligi ya Tano Kwa ubora Afrika ni kichekesho kikubwa kama Waamuzi kama hawa watabakia viwanjani.

Ubora wa Ligi yetu lazma iendane na ubora wa Waamuzi na isiwe team hiyo hiyo moja tu kupewa faida na Marefarii,Goli halali linakataliwa kisha Wanaenda kupewa Clear offside bila haya wala aibu.

Imagine kati ya mechi tano walizocheza tatu ni maumivu kwa wapinzani wao.

Kitu kimoja msichojua, wao hawajali na tunacholalamikia pembeni pembeni hususan mitandaoni, wataendelea kukusanya points za dhulma na tukija kustuka ubingwa huo hapo kwao.

Lazma tuseme kwa nguvu bila kumuonea mtu haya,tuiambie Mamlaka wazi wazi kuhusu ubabaifu uliokithiri wa udhalimu unaoendelea na tusijali matokeo ya adhabu zao, maana tutakuwa tunataka haki ya ligi bora isiyo na dhulma.

Tukiwa Soft nawaambia wazi wazi hakuna hatua zitachukuliwa kukomesha hizi mbeleko, tunapaswa kusema public kwa Sauti kuu yenye kudai haki ya usawa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’