Kiungo Jonas Mkude ni miongoni mwa wachezaji waliorejea mazoezini jana kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Oktoba 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mkude alikosekana kikosini kwa wiki kadhaa kutokana na changamoto ya majeraha
Yanga imeanza maandalizi mapema ikiwakosa wachezaji 10 ambao wameitwa timu za Taifa
Wachezaji walio kwenye majukumu ya timu za Taifa ni Djigui Diarra, Metacha Mnata, Dickson Job, Ibrahim Bacca na Bakari Nondo Mwamnyeto
Wengine ni Nickson Kibabage, Khalid Aucho, Mudathir Yahya, Stephane Aziz Ki na Clement Mzize










ADVERTISE HERE