Kikosi cha Yanga Princess kinachonolewa na kocha Charles Haalubono kinaendelea na mazoezi uwanja wa Uhuru kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Wanawake 'Serengeti Lite'
Ikiwa sehemu ya maandalizi yake, Yanga Princess leo ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu uliopita JKT Queens. anga Princess iliibuka na ushindi wa mabao 2-0
JKT Queens ndio mabingwa wa Afrika Mashariki kwa soka la Wanawake wakitarajiwa kuwakilisha ukanda huu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kutimua vumbi kuanzia Novemba 05 hadi Novemba 19 huko Ivory Coast
Kikosi cha Yanga Princess kimeendelea kuimarika malengo ya msimu huu yakiwa ni kutwaa ubingwa
ADVERTISE HERE