Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amesema Yanga ni lazima ijiandae kikamilifu kuweza kutinga hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho.
Yanga itakuwa nyumbani April 07 kuikabili Welayta Dicha ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza wa kusaka tiketi ya kutinga makundi.
Wapo wanaoibeza Welayta Dicha kwa kuwa inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ya kwao Ethiopia ikiwa imecheza michezo 15 na kujikusanyia alama 19 lakini Lwandamina amesema mpira umebadilika siku hizi.
"Tuliopopangiwa na St Louis wengi waliamini utakuwa mchezo mwepesi lakini haikuwa hivyo. Hata mchezo dhidi ya Township Rollers wengi waliamini tungefuzu kwa urahisi lakini matokeo yakawa tofauti," amesema Lwandamina ambaye anatarajiwa kurejea Jumatatu kutoka mapumzikoni kwao Zambia.
"Tunahitaji kujiandaa kikamilifu ili tuweze kufuzu. Dicha kufika hatua hii wamepambana, sio timu ya kubeza"
Welayta Dicha ilicheza na Zimamoto kwenye mchezo wa raundi ya awali na kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 2-1 kabla haijaiondoa Zamalek kwa mikwaju ya penati kwenye raundi ya kwanza baada ya matokeo ya 3-3.
Kabla ya kuikabili Dicha April 07, Yanga itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Singida United April 01 kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA (ASFC)

ADVERTISE HERE