Uongozi wa Njombe Mji FC umesema haujapokea taarifa yeyote kuhusu mabadiliko ya terehe ya mchezo dhidi ya Simba kupangwa kucheza Aprili 3 2018.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Njombe Mji, Hassan Macho, amesema kuwa taarifa zinazosambazwa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari, mpaka sasa hazina uthibitisho wowote.
"Kanuni ya ligi kuu inatamka kwamba taarifa za mabadiliko ya mchezo zitatolewa kwa klabu siku 14 kabla ya mchezo husika. Timu ya Njombe mji haijapokea taarifa kuhusu mchezo huo kuchezwa tarehe 3.4.2018" ameeleza.
"Hii itakuwa njia ya kutuondoa kwenye ligi, haiwezekani tukacheze Shinyanga siku mbili halafu turudi Njombe kisha turudi tena Shinyanga siku mbili baadae.
"Kanuni inataka tupate taarifa siku kumi na nne, hata tukipewa taarifa kesho basi siku hizo hazikidhi kwa mujibu wa kanuni" amesema Macho.
Njombe Mji itakuwa mkoani Shinyanga March 30 kuikabili Stand United kwenye mchezo wa kombe la FA kisha kwa mujibu wa ratiba ya TFF itatakiwa kurejea Njombe kuikabili Simba April 03 halafu itasafiri tena kwenda mkoani Shinyanga kuikabili Stand United kwenye mchezo wa ligi April 08.
Ratiba ya awali ilikuwa ikionyesha kuwa Njombe Mji ingebaki mkoani Shinyanga baada ya mchezo wao wa kombe la FA March 30 kusubiri mchezo wa ligi uliopangwa kupigwa April 08 dhidi ya haohao Stand United

ADVERTISE HERE