Nkomola awapania Welayta Dicha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Mar 2018
Nkomola awapania Welayta Dicha
Baada ya kukakaa nje kwa muda mrefu, mshambuliaji wa Yanga, Yohana Mkomola amesema ndoto yake ya kucheza mashindano ya kimataifa inatimia.

Nkomola aliumia kifundo cha mguu katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting na kulazimika kukaa nje kwa muda mrefu, lakini sasa ameanza mazoezi na kikosi cha Yanga.

Nkomola alisema kwa sasa anafanya mazoezi ya nguvu tofauti na awali ambapo yalikuwa mepesi, hatua hiyo inampa imani ya kucheza mechi ijayo ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Welayta Dicha ya Ehiopia.

"Hakuna mchezaji asiyetamani kuchangia mafanikio ya timu yake, nilikuwa naumia kuikosa mashindano hayo wakati timu yangu, ikicheza mechi ya Ligi Mabingwa Afrika, angalau napata moyo naweza nikacheza shirikisho,"

"Michuano hiyo inamsaidia mchezaji kuonekana nje, ni fursa ya kupanua ajira yangu, kwa umri wangu naona ni wakati mwafaka wa kujituma ili niweze kucheza soka la kulipwa," alisema.

Mbali na kutamani kucheza mashindano ya kimataifa ,alisema ndoto yake ni kuona Yanga inatwaa ubingwa akiwa na kikosi hicho, ili aweze kuwa katika rekodi ya kukumbukwa na wachezaji watakaokuja nyuma yake.

"Hata sisi tumekuta rekodi za wachezaji wakongwe, naamini walikuwa kama sisi ndio maana natamani kufanya kitu kwa nafasi hii niliopata kucheza klabu ya Yanga," alisema chipukizi huyo.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’