Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amepigwa fainali ya Tsh Milioni 1 na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi ya Bodi ya Ligi akidaiwa kumkejeli mwamuzi wa mchezo wa ligi kuu kati ya Singida BS dhidi ya Simba, Tatu Malogo
Taarifa iliyotolewa na Kamati hiyo imebainisha kuwa Kamwe alifanya kosa hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Aidha mwamuzi msaidizi wa mchezo tajwa amesimamishwa mechi tano kwa kosa la kushindwa kutafsiri vyema sheria za soka
Kamati hiyo pia imemsimamisha mwamuzi msadizi namba mbili wa mchezo kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Simba kwa kushindwa kutafsiri sheria za soka
Yanga pia imetozwa faini Tsh Milioni 1 kwa kosa la mashabiki wake kurusha chupa uwanjani katika mchezo dhidi ya Ihefu Fc
Wananchi pia wametozwa faini ya Tsh Milioni 1 kwa kosa la maafisa wake wa benchi la ufundi kuonekana mara kadhaa wakipinga maamuzi ya waamuzi wa mchezo dhidi ya Ihefu Fc