Wanachama na Mashabiki wa Yanga wamemchangia Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ali Kamwe kiasi cha Tsh Milioni 1 kwa ajili ya kulipia faini aliyopigwa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi
Kamwe aliadhibiwa na Kamati hiyo kwa tuhuma za kumkejeli mwamuzi Tatu Malogo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii baada ya mchezo kati ya Singida BS dhidi ya Simba ambao uligubikwa na lawama nyingi kwa waamuzi
Mwanachama maarufu wa klabu ya Yanga Jimmy Msindo 'Kindoki' aliendesha ukusanyaji wa michango hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandano wa Instagram na fedha hizo kupatikana baada ya saa 4

Kindoki amesema dhumuni la kuendesha harambe hiyo ni kuonyesha kuwa Wanayanga wako pamoja na Afisa habari wao na hawatanyamaza kukemea maamuzi ya upendeleo pasipo kuogopa kupigwa faini
Waamuzi wasaidizi katika mechi mbili ambazo Simba walifunga mabao yenye utata dhidi ya Prisons na Singida BS wote wamefungiwa mechi tano lakini mwisho wa siku bado Simba itaendelea kubaki na alama sita ambazo adhabu hizi zinaashiria hawakuzipata kihalali
Kindoki amesema waamuzi wanapaswa kuchezesha mechi zote kwa usawa pasipo kupendelea timu yoyote ili mwisho wa msimu bingwa apatikane kihalali
Wakati Wananchi wakichanga Tsh Milioni 1, msanii wa Bongo Fleva Bilnas 'Mzee wa Maokoto' nae ameahidi kuilipa faini hiyo aliyopigwa Kamwe