Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi Avic Town kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc
Mchezo huo wa mzunguuko wa sita utapigwa Jumatatu, Oktoba 23 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga inajiandaa kikamilifu ili kuhakikisha inaondoka na alama zote tatu
Pamoja na kuwa na rekodi nzuri katika mechi dhidi ya Azam Fc zilizopigwa karibuni, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema mchezo utakuwa mgumu na wenye ushindani hivyo ni lazima wajiandae sawasawa
Alama tatu kwa Yanga katika mchezo huo, zitawahakikishia Wananchi kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kabla ya mchezo mwingine dhidi ya Singida BS utakaopigwa Oktoba 27
ADVERTISE HERE