Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa jana alitoa ufafanuzi utaratibu ambao utatumika msimu huu kupata bonus ya goli la Mama
Kama ilivyokuwa msimu uliopita, goli la Mama linaendelea, bonas maalum anayotoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kila goli linalofungwa na timu za Tanzania zinazoshiriki michuano ya KimataifaΒ
Hata hivyo Msigwa amesema kuwa msimu huu bonus hiyo itatolewa pale tu timu husika imeshinda mchezo na sio kutoka sare au kufungwa
Maana yake ni kuwa kama umefunga lakini hukupata ushindi basi unakosa sifa ya kupata bonus ya goli la Mama
Ndicho kilichotokea uwanja wa Benjamin Mkapa jana kwenye mchezo wa AFL licha ya Simba kufunga mabao mawili, kwa kuwa ililazimishwa sare dhidi ya Al Ahly haikupata bonus ya Tsh Milioni 10 kwa kila goli