Baada ya mapumziko ya takribani wiki tatu, burudani kwa Wananchi inarejea kesho Jumatatu pale uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc
Mtanange huo wa kukata na shoka, utapigwa majira ya saa 12:30 jioni. Burudani imerejea kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kuanza msimu kule Chamazi
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka Wananchi wanunue tiketi zao mapema ili wapate kushuhudia burudani ya timu yao waliyoikosa kwa wiki kadhaa
Hii ni dabi ya Dar es salaam, mechi ambayo Yanga inazihitaji alama zote tatu ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi


ADVERTISE HERE