Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc yamekamilika
Gamondi amesema vijana wake wako tayari kwa mechi nne mfululizo za ligi ukiwemo mchezo wa kesho dhidi ya Azam Fc na malengo ni kushinda
"Tunafahamu tunakwenda kupambana na timu ngumu Azam Fc, moja ya timu bora hapa Tanzania lakini sisi tuna malengo ambayo tunahitaji kuyatimiza"
"Nafurahi tumerejea katika uwanja wa Benjamin Mkapa, ari ya kikosi iko juu, kila mmoja ana shauku kubwa ya kucheza mchezo huo"
"Zipo changamoto za majeruhi, kuna wachezaji watatu ambao wana majeraha madogo lakini nafikiri baada ya mazoezi ya mwisho leo tutakuwa na wachezaji 20 kwa ajili ya mchezo huo," alisema Gamondi
Gamondi amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi katika dimba la Benjamin Mkapa kuishangilia timu yao kwani anaamini shabiki ni mchezaji wa 12 uwanjani
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, winga Skudu Makudubela amewataka mashabiki wa Yanga wajtokeze kwa wingi uwanjani kwani wamewaandalia burudani itakayoambatana na ushindi mnono
"Kama kocha alivyosema, tunawahitaji mashabiki waje kwa wingi kwani wao ni wachezaji wa 12. Tunafahamu mashabiki wetu wanahitaji burudani ambayo ni kushangilia magoli hivyo tunawaahidi tutawapa burudani hiyo," alisema Skudu