Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amewapongeza wachezaji wenzake kwa kupambana na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Aziz Ki leo alikuwa nyota wa mchezo akifunga mabao matatu 'hat-trik' katika mchezo huo ambao Yanga ililazimika kutokea nyuma kwa mabao 2-1 na kupata ushindi huo
Aziz Ki amesema ushindi huu ni matokeo ya upambanaji wa pamoja kwa wachezaji wote
"Nina furaha kubwa kwa kuisaidia timu yangu kuibuka na ushindi huu leo, hata hivyo ni matokeo ya timu"
"Kila mmoja ameshiriki katika mafaniko haya, mimi nilikuwa na jukumu la kufunga tu lakini nimepokea pasi kutoka kwa wenzangu"
"Hivyo ushindi huu nautoa kwa timu nzima kwani tumepambana sana kufanikisha malengo haya," alisema Aziz Ki
Mabao matatu aliyofunga Aziz Ki leo yamemfanya awe kinara katika mbio za ufungaji bora akifikisha mabao sita
Kwa wastani Aziz Ki amefunga bao katika kila mchezo wa ligi kuu msimu huu