Pacome Zouzoua, fundi mmoja

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Oct 2023
Pacome Zouzoua, fundi mmoja

Wananchi wanaendelea kufurahia kiwango bora kinachoonyeshwa na wachezaji wao msimu huu katika michuano mbalimbali

Jana Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Azam Fc katika ligi kuu ya NBC na kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi

Ni mchezo ambao wachezaji wa Yanga walimwagika jasho jingi kuweza kupata ushindi huo

Miongoni mwa wachezaji waliokonga nyoyo za Wananchi ni Pacome Zouzoua, MVP wa ligi kuu ya Ivory Coast msimu uliopita

Pacome ni kiungo mshambuliaji mwenye maarifa makubwa ya kucheza mpira, jana aliwapa wakati mgumu walinzi wa pembeni wa Azam Fc kabla ya kuingia kwenye eneo la kiungo baada ya Mudathir kutoka

Akiwa na mpira ni ngumu kubaini nini anataka kufanya  lakini pia jana alionyesha yuko fit na anaweza kung'ara katika mechi ngumu

Msimu huu Pacome ameifungia Yanga mabao matatu kwenye ligi na kutoa pasi mbili za mabao

Lakini pia ana bao moja kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika

Sasa amejihakikishia nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha Miguel Gamondi, Wananchi watarajie mambo makubwa zaidi kutoka kwake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
29m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
35m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’