Mlinzi wa kulia wa Yanga Yao Kouassi yuko kamili kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida BS ambao utapigwa Ijumaa, Oktoba 27 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Yao alikosa mchezo uliopita dhidi ya Azam Fc uliiopigwa dimba la Mkapa Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 3-2
Kinara huyo wa 'assist' ligi kuu ya NBC alipewa mapumziko na kocha Miguel Gamondi ili kuhakikisha afya yake inakaa sawa sawa ili kuweza kutumika katika mechi mbili muhimu zinazofuata dhidi ya Singida BS na Simba
Nyota mwingi aliyerejea kikosini kutoka kwenye majeraha ni Farid Mussa
Yanga inaendelea na maandalizi Avic Town kujiandaa na mchezo dhidi ya Singida BS Wananchi wakipania kuvuna alama tatu ili kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi
ADVERTISE HERE