Matchday : Yanga vs Singida BS, NBC PL, Oct 27

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Oct 2023
Matchday : Yanga vs Singida BS, NBC PL, Oct 27

Kikosi cha Yanga majira ya saa 12 jioni kitashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Singida BS katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Azam Fc, Wananchi wanarudi tena dimba la Mkapa kusaka alama nyingine tatu ambazo zitawaimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi

Hata hivyo wanakutana na Singida BS iliyo katika kiwango bora sasa baada ya kuanza ligi kwa kusuasua

Ni mchezo wa pili mfululizo Yanga inatumia dimba la Mkapa ambao ndio uwanja wa nyumbani wa Wananchi

Mchezo huu utakuwa sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Yanga kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa wiki ijayo, Novemba 05

Ushindi kwa Yanga utawahakikishia kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kabla ya kukutana na Simba ambao hata hivyo wana mechi moja ya kiporo ambayo huenda ikachezwa kabla vigogo hao wa soka nchini kukutana

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi dimba la Mkapa jioni ya leo akiahidi vijana wake kutoa burudani itakayoambatana na ushindi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’