Baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki, kikosi cha Yanga leo kinaingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba
Mchezo huo utapigwa Jumapili, Novemba 05 katika uwanja a Benjamin Mkapa, saa 11 jioni
Yanga inaingia mawindoni ikiwa na dhamira moja tu, kushinda mchezo huo ili kuianza rasmi safari ya kutetea taji la Ligi Kuu kwa msimu wa tatu mfululizo
Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 18 sawa na Simba lakini Yanga ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga
Kama Yanga itashinda mchezo dhidi ya Simba basi itakuwa na uhakika wa kubaki kileleni mwa msimamo wa Ligi hata kama Simba watashinda mchezo wao wa kiporo
ADVERTISE HERE