Jumapili Novemba 05 2023 mchezo wa kwanza wa dabi ya Kariakoo Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba dhidi ya Yanga utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Simba watakuwa wenyeji wa mchezo huo utakaopigwa saa 11 jioni
Viingilio vya mchezo huo tayari vimetangazwa ambapo majukwaa ya Mazunguuko kiingilio ni Tsh 5,000/-
Machungwa ni Tsh 10,000/- wakati VIP C ni Tsh 20,000/- VIP B ni Tsh 30,000/- na VIP A ni Tsh 40,000/- Tiketi za Platinum ni Tsh 150,000/-

Yanga inazihitaji alama zote tatu za mchezo huu ili kujisimika kileleni mwa msimamo wa ligi
Wananchi wameaswa kununua tiketi zao mapema ili kuhakikisha Yanga inapata sapoti kubwa ya mashabiki katika mchezo huo ambao Yanga iko ugenini
ADVERTISE HERE